Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agoma kumshtaki mumewe kwa kumnajisi mwanaye, adai atamwombea

Mke Pic Agoma kumshtaki mumewe kwa kumnajisi mwanaye, adai atamwombea

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mwanamke mmoja huko Mombasa ameshangaza watu kwa kukataa kumripoti mume wake ambaye amemlawiti binti yao mwenye miaka mitatu.

Kwa mujibu wa kituo cha habari ‘Tuko’ wameeleza kwamba mjomba wa mtoto huyo Joseph Kithi amedai kuwa mtoto huyo alilawitiwa na baba yake mzazi Ijumaa, Machi 31 nyumbani kwao Bamburi, Kaunti ya Mombasa.

Lakini juhudi za kumshawishi mama yake huyo kuripoti tukio hilo kituo cha polisi ziligonga mwamba.

Kulingana na Kithi, mwanamke huyo amekataa kumchukulia mumewe hatua akisema kwamba akitoa taarifa kuhusu tukio hilo alilofanya mume wake, atakosa huduma.

Kithi aliongeza kuwa mtuhumiwa alimlawiti mtoto huyo bafuni alipokuwa akimuogesha. "Siku iliyofuata mtoto huyo alianza kulalamikia maumivu kwenye sehemu zake za siri na alipohojiwa na mama yake alikiri kulawitiwa na baba yake wakati akimwogesha na alimtishia asiseme neno lolote kwa mama yake," amesema.

Mama wa mtoto huyo amesema kuwa bado hajampeleka mtoto wake hospitalini kwa kuwa mtuhumiwa ndiye mlezi pekee anategemewa kutafuta riziki katika familia hiyo.

"Ni kweli ila naogopa akiwekwa selo polisi hakuna mtu wa kulea familia yangu. Hii ni kwa sababu nilijifungua kwa upasuaji na kwa sasa siwezi kufanya kazi," amebainisha.

Mwanamke huyo amesema alishauriwa na watu wake wa karibu kumwombea mumewe badala ya kwenda kutoa taarifa polisi.

"Siwezi kuongea kwa muda mrefu kwa sababu nimetoka kanisani baada ya kunipigia simu. Ninahudhuria ibada kwa sasa. Nilikwenda kumwomba Mungu atoe pepo waliomfanya atende kitendo hicho," ameeleza.

Mtoto huyo ambaye kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa bibi yake lakini hana uwezo wa kuzuia mkojo kwa sababu bado hajapatiwa matibabu.

Chanzo: mwanachidigital