Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungua kesi Mahakamani kupinga usajili laini za simu

Sim Card Afungua kesi Mahakamani kupinga usajili laini za simu

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Karanja Matindi, raia wa Kenya anayeishi Uingereza ameifungulia mashtaka Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwa kuagiza watumiaji wote wa laini za Simu kujisajili upya akisema ni kinyume cha Katiba.

Matindi anasema maamuzi hayo ya kujisajili upya kwa kufichua idadi ya namba za Simu, taarifa za mtumiaji na kutumia picha za wateja ni kinyume cha Sheria na inakiuka Haki na Katiba, na kuitaka Mahakama izuie na kuagiza picha za wateja zifutwe.

CA ilitoa tangazo kuwa laini ambazo hazijasajiliwa hadi kufikia Aprili 15, 2022 zitafungiwa. Hakimu ameipitisha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza akutane na CA na Kampuni za Mawasiliano ndani ya siku saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live