Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika yarekodi kiwango cha juu cha ukatili

WANAWAKE WEB Afrika yarekodi kiwango cha juu cha ukatili

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa unasema kwamba Wanawake na wasichana barani Afrika wako katika hatari kubwa ya kuuawa na wapenzi wao wa karibu au wanafamilia wengine, zaidi ya mahali pengine popote duniani.

Taarifa ya UN Inasema bara hili lina kiwango cha juu cha unyanyasaji dhidi ya wanawake, ikilinganishwa na ukubwa wake wa idadi ya wanawake.

Mwaka 2021, takriban wanawake na wasichana 45,000 duniani kote waliuawa na wapenzi wa karibu au wanafamilia wengine.

Hii inamaanisha kuwa zaidi ya wanawake au wasichana watano huuawa kila saa na mtu katika familia yake.

Ripoti iliyotolewa kwa pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) na UN Women, inasema hata kama idadi hiyo inashangaza, kiwango halisi cha mauaji kinaweza kuwa kikubwa zaidi.

Kwa idadi kamili, Afrika ilikuwa nni ya pili kwa  juu zaidi ya mauaji ya wapenzi wa karibu wa  au mauaji yanayohusiana na familia, yakiwa 17,200, huku Asia ikiongoza kwa visa 17,800. Amerika ilikuwa na visa 7,500 na 2,500 barani Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live