Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika yaongoza kwa kusitisha mikataba na China

Afrika Sauzi ..jpeg Afrika yaongoza kwa kusitisha mikataba na China

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imesitisha mkataba wa Dola Bilioni 2.2 (Tsh. Trilioni 5.1) wa Kampuni ya CHEC ya China kujenga reli ya Standard Gauge Railway (SGR) ya Kilometa 273 kutoka Malaba hadi Kampala kutokana na mvutano wa kimaslahi.

Hivyo, Uganda imeingia makubaliano ya awali na Kampuni ya Uturuki ambayo ndiyo inayojenga SGR ya Tanzania ikidaiwa gharama zao zinaweza kuwa ni Dola Bilioni 1.5 hadi 1.72 (Tsh. Trilioni 3.5 hadi 4).

Huo ni mwendelezo mbaya wa mikataba ya China katika mataifa mbalimbali kwa hivi karibuni. Ghana pia ilisitisha mkataba wa matengenezo ya mfumo wa kuangalia magari.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ameagiza kupitiwa kwa mkataba wa madini uliosainiwa Mwaka 2008 akidai haridhishwi na utendaji.

Mwaka 2022, Kenya ilitisisha mkataba wa ujenzi wa SGR.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins katika utafiti wa China-Afrika wa Mwaka 2000 - 2019, China ilisaini mikataba ya 1,141 ya kutoa mikopo yenye thamani ya Dola 153.

Aidha, Mexico pia imefuta mkataba wa ujenzi wa treni ya mwendokasi. Ethiopia nayo imefuta mkataba wa gesi, mafuta uliosainiwa Mwaka 2013.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live