Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika kusini yatoa tahadhari ongezeko la maafa Gaza

Zaidi Ya Watu 30,000 Wameuawa Gaza, Hamas Wasema Afrika kusini yatoa tahadhari ongezeko la maafa Gaza

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini jana alitahadharisha kuwa maafa ya kutisha yatashuhudiwa Ukanda wa Gaza iwapo mazungumzo kuhusu kuwaachia huru mateka na kusitisha vita katika eneo hilo yatafeli.

Naledi Pandor aliiambia kanali ya habari ya Afrika Kusini ya SABC kuwa wamemtuma balozi wao Umoja wa Mataifa kufanya juhudi zote ili kuzungumza na mabalozi wengine na kutilia mkazo juu ya kupasishwa azimio la dharura kwa ajili ya kusimamisha vita Ukanda wa Gaza.

Pandor amesema: Kwa sasa tunafikiri kwamba kila mtu anapaswa kuzingatia usitishaji vita haraka iwezekanavyo na kuongeza kuwa dunia itashuhudia maafa ya kutisha na hata zaidi ya hiki kinachotokea huko Gaza iwapo vita havitasitishwa katika eneo hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ameendelea kusema: "Natamani ningewaambia watu wa Palestina na Waislamu wote 'Ramadhan Mubarak' lakini kwa watu wa Palestina naona hali mbaya ikiwa ulimwengu hautashughulikia suala hili la dharura la kusitisha vita haraka iwezekanavyo."

Afrika Kusini imelaani vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza; ambapo mwaka jana nchi hiyo ilifungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ huko The Hague Uholanzi ikiituhumu Israel kwa mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina wa Ukanda wa Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live