Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika inapendekeza ushuru kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Afrika Inapendekeza Ushuru Kimataifa Kupambana Na Mabadiliko Ya Tabianchi Afrika inapendekeza ushuru kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Afrika wamependekeza mfumo wa kimataifa wa ushuru wa kaboni katika tamko la pamoja.

Azimio la Nairobi lilihitimisha Mkutano wa siku tatu wa hali ya hewa wa Afrika katika mji mkuu wa Kenya.

Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano, ilitaka wachafuzi wa mazingira watoe rasilimali zaidi kusaidia mataifa maskini.

Wakuu wa nchi za Afrika walisema watatumia azimio hilo kama msingi wa msimamo wao wa mazungumzo katika mkutano wa kilele wa COP28 wa Novemba.

Mkutano wa Kilele wa mabadiliko ya tabianchi wa Afrika ulitawaliwa na mijadala kuhusu jinsi ya kuhamasisha ufadhili ili kukabiliana na hali ya hewa inayozidi kuwa mbaya, kuhifadhi maliasili na kuendeleza nishati mbadala.

Afrika ni miongoni mwa mabara yaliyo hatarini zaidi kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini kulingana na watafiti, inapokea tu takriban 12% ya karibu $300bn (£240bn) katika ufadhili wa kila mwaka inaohitaji kustahimili.

Azimio la Nairobi liliwataka viongozi wa dunia "kuunga mkono pendekezo la mfumo wa kimataifa wa ushuru wa kaboni ikiwa ni pamoja na ushuru wa kaboni kwenye biashara ya mafuta, usafiri wa baharini na usafiri wa anga, ambayo inaweza pia kuongezwa na ushuru wa shughuli za kifedha duniani".

Ilisema hatua kama hizo zitahakikisha ufadhili mkubwa kwa uwekezaji unaohusiana na mabadiliko ya hali hewa na kuzuia suala la kupanda kwa ushuru kutoka kwa shinikizo la kijiografia na siasa za ndani.

Takriban nchi zaidi ya 20 kwa sasa zinatoza kodi kwenye kaboni, kulingana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), lakini wazo la mfumo wa kimataifa wa kodi ya kaboni limeshindwa kupata msukumo mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live