Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yazitaka nchi nyingine kuibana Israel

Bunge La Israel Limekataa Pendekezo La Kuundwa Kwa Taifa La Palestina Afrika Kusini yazitaka nchi nyingine kuibana Israel

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi, Vusi Madonsela, amezitaka nchi zote duniani kutoa ushahidi katika kesi ya nchi yake dhidi ya Israel huko The Hague na kuuwajibisha utawala huo pandikizi kwa jinai na mauaji yake ya umati katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa upande wake, shirika la habari la FARS limetangaza kuwa, kumnukuu Balozi Madonsela akisema: "Tunatarajia kwamba mwisho wa kesi hiyo, Mahakama ya Kimataifa ya Haki itatangaza kwamba kuendelea kukaliwa kwa ardhi za Palestina na Israel ni kinyume cha sheria na lazima kukomeshwe."

Vile vile ametoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazofuata za kisheria na kwamba kesi hiyo itapelekwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ili kukomesha ubaguzi wa rangi unaofanywa na Wazayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ya The Hague siku ya Jumatatu ilianza wiki ya vikao vya kusikiliza mashauri ya kisheria ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala ghasibu wa Israel ambapo majaji wa mahakama hiyo wanatakiwa kusikiliza hoja za nchi 50 kuhusu shauri hilo.

Siku ya Jumanne, siku ya pili ya kusikilizwa katika Mahakama ya The Hague, Madonsela alisema kuwa "Israel inatenda jinai kubwa zaidi za ubaguzi wa rangi katika maeneo ya Wapalestina kuliko jinai za mwaka 1994 zilizofanywa na Makaburu nchini Afrika Kusini."

Balozi wa Afrika Kusini jana Jumamosi alizikaribisha nchi wanachama wa Mkataba wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari kushiriki katika vikao vya Mahakama ya The Hague na kuwasilisha maoni yao pamoja na ushahidi walio nao ili kuionyesha mahakama hiyo kuwa Israel imetenda jinai na uhalifu mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live