Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yatoa wito kususia bidhaa za Israel

Waziri Kusini Palestina Afrika Kusini yatoa wito kususia bidhaa za Israel

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi kususia bidhaa za Israel, akieleza kuwa watu wa Palestina wanahitaji vifaa vya matibabu.

Naledi Pandor amewataka mamilioni ya watu kutoa michango yao kwa kutoa misaada na kuisafirisha hadi kwenye mpaka wa Misri kwa sababu ya mashambulizi ya kikatili yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Afrika Kusini ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa "Matatizo ya Kibinadamu" ulioandaliwa na Shirika la Kazi la Umoja wa Kitaifa, amelaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, akisisitiza kwamba chanzo cha mzozo huu ni "kuendelea kuzikalia kinyume cha sheria ardhi za Palestina."

Naledi Pandor pia melaani mzingiro wa nchi kavu, baharini na angani uliowekwa na Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kwa miaka kadhaa sasa, akibainisha kwamba Wapalestina "hawana uhuru wa kutembea", "wananyimwa uhuru wa kuingia na kutoka katika ardhi zao, na haki ya watoto kupata elimu."

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Afrika Kusini ameendelea kuhoji huku akiwa amevaa skafu ya Kipalestina kwamba: "Kwa nini inaruhusiwa kwa mwandishi wa habari wa Palestina kuuawa, na sio kwa mwandishi wa Canada?" Aidha amekosoa kimya cha Wamagharibi kuhusu mauaji ya Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa Al Jazeera, ambaye amesema: "aliuawa mbele ya macho ya walimwengu na vyombo vya habari."

Naledi Pandor amekariri msimamo wake wa kukataa kabisa Israel kuwa mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika, akisisitiza kwamba "Afrika Kusini haitakubali kamwe suala hili."

Awali, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alieleza uungaji mkono wakwe kwa mapambano ya kupigania uhuru ya Palestina, huku Ukanda wa Gaza ukiendelea kuzingirwa mzingiro na kushambuliwa vikali kwa mabomu ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live