Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yatangaza kusimamisha shughuli zote nchi nzima kwa wiki tatu kutokana na corona

100087 SA+PIC Afrika Kusini yatangaza kusimamisha shughuli zote nchi nzima kwa wiki tatu kutokana na corona

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza nchi hiyo kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa wiki tatu, ambapo shughuli zote zitasimama kasoro zile za muhimu kwa jamii. Ramaphosa amesema kuwa agizo hilo limeanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 24, 2020 ambapo watu wote hawataruhusiwa kutoka nje ya nyumba zao isipokuwa kwa sababu za lazima. Amesema wiki hizo tatu zitakuwa ni siku muhimu zitakazotumiwa kupambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona. Ripoti kutoka nchini humo imeeleza kuwa hadi sasa jumla ya watu 402 wameripotiwa kukutwa na virusi vya ugonjwa wa corona. Rais Ramaphosa alihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni na kusema kuwa, katika kipindi nchi hiyo ikiwa chini ya uangalizi huo, watu hawataruhusiwa kutoka kwenye nyumba zao ila tu kwa sababu za ulazima na kwa uangalizi wa hali ya juu sana wa mamlaka. Aliongeza kuwa, maduka yote na biashara zitafungwa isipokuwa zile zinazotoa huduma za umuhimu. Kwa watu ambao hawana makazi ya kuishi amesema watapewa malazi ya muda mfupi yaliyoandaliwa kwa ajili yao. Aliongeza kuwa wahudumu wa afya na wafanyakazi wa sekta ya ulinzi na usalama hawatahusika katika karantini hiyo. “Tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kupunguza idadi ya maambukizi na kupunguza kasi yake kwa muda mrefu,” alisema Rais Ramaphosa.

Chanzo: mwananchi.co.tz