Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yataka kikosi cha UN kuwalinda raia wa Gaza

Wapalestina Kumi Na Saba Waliuawa Katika Mapigano Ya Ukingo Wa Magharibi Afrika Kusini yataka kikosi cha UN kuwalinda raia wa Gaza

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afrika Kusini Jumatatu imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kutuma Ghaza kikosi cha askari wake haraka iwezekanavyo ili kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imesema katika taarifa yake kuwa idadi ya raia waliouawa, hasa watoto, inahitaji ulimwengu kuonyesha kuwa unafuatilia jambo hilo kwa makini na kuwajibika kimataifa.

Hayo yanajiri huku utawala wa kibaguzi wa Israel ukiendeleza mashambulizi yake makali ya anga na makombora dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina huku wanajeshi wakitumia vifaru na zana nyiingine nzito kupanua uvamizi wao wa nchi kavu.

Israel ilitangaza vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas, baada ya shambulio la Kimbunga cha Al Aqsa Oktoba 7 ambapo wanamuqawama walivuka mpaka kutoka Ukanda wa Ghaza na kuwaua takriban Wazayuni 1,400 wakiwemo wanajeshi wa Isreal. Hujuma ya kinyama ya Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza

Pamoja na hayo Wizara ya Afya katika eneo la Ghaza inasema zaidi ya raia wa kawaida elfu nane wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wameuawa huko Gaza tangu wakati huo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa misaada ya kibinadamu (OCHR) inasema waokoaji wanahangaika na kusumbuka sana katika kuwafikia waathirika wanaohitajia msaada wao. Kuna ongezeko la wito wa kimataifa kwa ajili ya raia wa Palestina, walionaswa kati ya pande zinazopigana, kulindwa.

Afrika Kusini kwa muda mrefu imekuwa mtetezi wa amani katika eneo hilo na inalinganisha masaibu na mateso ya Wapalestina na hali yake wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Hata hivyo, wito wake wa kutaka kikosi cha ulinzi cha Umoja wa Mataifa kipelekwe Ghaza, umeenda mbali zaidi katika uungaji mkono wake huo kuliko mataifa mengine mengi, ambayo baadhi yametaka kusitishwa mapigano au kufunguliwa vifuko kwa ajili ya kufukishwa misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live