Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yashangazwa na maamuzi ya Uingereza kuhusu wasafiri

Arivald Afrika Kusini yatilia mashaka maamuzi ya Uingereza

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Uingereza kuliweka taifa la Afrika Kusini katika orodha za nchi ambazo raia wake lazima wafikie katika Karantini maalumu pindi tu waingiapo nchini humo 'Red list' inaelezwa kuwa Serikali ya Afrika Kusini imeingiwa na mashaka makubwa juu ya maamuzi hayo.

Hatua hiyo inawalazimu raia wote wanaotoka nchini humo kukaa katika hoteli maalumu ambazo Serikali ya Afrika Kusini imezilalamikia kuwa ni ghali sana kuweza kumudu kwa siku 14 kwa mujibu wa sera za afya.

Wakati serikali ya Afrika Kusini ikijitahidi kuinua tena Sekta ya utalii ambayo imezorota kufuatia ugonjwa wa Corona unaotesa taifa hilo, hivyo hatua hiyo inaleta wasiwasi kwa watalii kutoka uingereza ambao wananuia kufika nchini humo kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii.

Aidha Sekta ya utalii nchini humo hutoa zaidi ya nafasi za ajira 700,000 kwa wananchi wa Afrika Kusini, hivyo jambo hilo linaashiria kuibuka kwa kundi kubwa la watu wasiokuwa na ajira nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live