Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yasema taarifa kumhusu mama aliyejifungua watoto 10 ni ya uwongo

747d90cb20c0dbf6 Afrika Kusini yasema taarifa kumhusu mama aliyejifungua watoto 10 ni ya uwongo

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ripoti kutoka kwa vyombo kadhaa vya habari zimebaini kuwa hamna rekodi yoyote kuwahusu watoto 10 wa TembisaTaarifa kuwahusu watoto 10 waliozaliwa kwa mpigo ambazo zilitikisa ulimwengu zinasemekana zilikuwa za uongo kufuatia uchungi wa serikali ya mkoaUchunguzi uliofanywa kwa mama huyo ulionesha kuwa hakuwa mjamzito na kwamba anapokea matibabu ya kiakiliHamna hospitali hata moja mkoani Gutaeng, Afrika Kusini ambayo ilirekodi kuzaliwa kwa watoto 10 kwa mpigo maarufu kama Tembisa 10 kulingana na ripoti ya mkoa huo.

Uchunguzi uliofanywa kwa Bi Gosiame Sithole, ambaye anadaiwa kuwazaa watoto hao, alionyesha kuwa hakuwa na ujauzito katika nyakati za hivi karibuni.

Kwa sasa Sithole anachunguzwa kiakili huku pia akipewa mwongozo wa ushauri katika hospitali.

Taarifa iliyotolewa na serikali huko Gauteng haikufichua ni kwanini hadithi hiyo ilibuniwa.

Hata hivyo, taarifa za Pretoria News zilishikilia kwamba Sithole alijifungua watoto hao kumi mnamo Juni 7, katika hospitali ya Steve Biko mjini Pretoria.

Kulingana na BBC News, chapisho hilo lilisema wafanyakazi katika hospitali hiyo walikuwa hawajajiandaa vyema na walituhumu kituo cha huduma ya matibabu na wahudumu wa afya huko Gauteng kwa kujaribu kuficha utepetevu wao kazini.

Taarifa ya hivi karibuni ya serikali zilifichua kwamba madai hayo kutoka kwa vyombo vya habari yalikuwa 'ya uwongo na yasiyokuwa na uthibitisho' na yalikuwepo tu ili kudunisha sifa ya SBAH na serikali ya Gauteng.

News24 iliripoti kuwa serikali ya Gauteng ilikuwa inapanga kumshtaki Piet Rampedi, mhariri wa Pretoria News.

Iliongeza kuwa ingependelea ikiwa taarifa ya hiyo ya uwongo kufutiliwa mbali na pia shirika hilo la habari liombe msamaha dhidi ya madai yaliyotolewa kuhusiana na serikali ya mkoa.

Awali, msemaji wa serikali ya Afrika Kusini alisema hamna ushahidi wowote kwamba Sithole alijifungua watoto 10 kwa mpigo.

Kulingana na taarifa ya Phumla Williams, waliisaka familia hiyo bila mafanikio.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke