Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yasema haina mipango ya kujiondoa ICC

Mnangagwa ZANU PF M.jpeg Afrika Kusini yasema haina mipango ya kujiondoa ICC

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaposa ametoa taarifa kwamba nchi yake haina mipango ya kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma kuhusu kuanzishwa na mchakato wa mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) kinyume na kauli aliyozitoa mwenyewe rais Jumanne.

Mwezi Agosti kikao cha ZRICS kinatarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini, na kwa hali ilivyo sasa rais wa Urusi anapaswa kukaribishwa.

Afrika Kusini inaitambua kisheria mahakama ya The Hague, ambayo ilitoa waranti ya kumkamata Vradimir Putin, na atatakiwa rasmi kutekeleza waranti (hatahivyo, hakuna vikwazo vinavyotolewa kwa wasiotekeleza waranti).

Ofisi ya rais inadai kwamba chama tawala cha African National Congress (ANC) kilikosea katika mazungumzo.

"Ofisi ya rais inataka kuweka wazi kwamba, Afrika Kusini bado imesalia kuwa mwanachama wa Sheria ya Roma. Hii inafuatia kutokamilika kwa kauli katika mazungumzo kwa vyombo vya habari yaliyofanywa na chama cha ANC," ilieleza taarifa iliyotolewa usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live