Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yalaani shambulio hospitali Gaza

Mzozo Wa Israel Na Palestina: Mabomu 6,000 Yaangushwa Gaza Afrika Kusini yalaani shambulio hospitali Gaza

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Afrika Kusini jana Jumatano ililaani shambulizi la anga la Israel katika hospitali ya al Maamadani inayoitwa Al-Ahli Baptist Hospital katikati ya Ghaza na kuua zaidi ya watu 500 na kuwajeruhi zaidi ya 1,000 wengine na imeitaja jinai hiyo kuwa ni uhalifu wa kivita.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kuisni imesema, hakuna maneno ya kuweza kubainisha kikamilifu namna Afrika Kusini inavyolaani shambulizi la Israel la kuriipua hospitali ya al Maamadani huko Ghaza.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kuwalenga raia katika kivita ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na za kibinadamu na Mikataba ya Geneva.

Shambulio la anga katika hospitali hiyo lilitokea Jumanne usiku ikiwa ni siku ya 11 ya jinai za Israel kwenye Ukanda wa Ghaza. Makundi ya kimataifa hasa yasiyo ya kiserikali na viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kulaani jinai hizo za Israel ikiwa ni pamoja na mashambulizi yake dhidi ya vituo vya afya, maskuli na nyumba za ibada na wamekuwa wakisisitiza kuwa Israel inakanyaga sheria za kimataifa na inafanya jinai za kivita. Zaidi ya watu 500 waliuawa shahidi kwa mkupuo mmoja katika shambulizi hilo la anga la Israel. Al-Ahli Baptist Hospital ya katikati mwa Ghaza kabla Wazayuni hawajaishambulia na kufanya mauaji ya kutisha ya mamia ya watu

Pretoria imekuwa ikipinga ukatili wa Tel Aviv katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Jana Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor alithibitisha habari zinazosema kwamba alizungumza kwa simu na viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas juzi Jumanne na kujadiliana nao njia za kuweza Afrika Kusini kuwafikishia misaada ya kibinadamu wananchi wa Ghaza.

Siku chache zilizopita pia, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alitangaza mshikamano wake na Wapalestina mbele ya jinai za kutisha zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina hao wasio na ulinzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live