Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yakabiliwa na hatua za kisheria kuhusu mzozo wa umeme

Afrika Kusini Yakabiliwa Na Hatua Za Kisheria Kuhusu Mzozo Wa Umeme Afrika Kusini yakabiliwa na hatua za kisheria kuhusu mzozo wa umeme

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Makundi ya upinzani nchini Afrika Kusini, chama cha wafanyakazi na wamiliki wa biashara wametishia kuishtaki serikali kutokana na kukatika kwa umeme nchini humo.

Wameipa serikali hadi Ijumaa kuweka nishati ya umeme kutengamaa la sivyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka wajibu wake wa kutoa umeme.

Wameandika barua ya madai kwa Waziri wa Mashirika ya Umma Pravin Gordhan na mtendaji mkuu wa kampuni ya shirika la serikali ya Eskom, Andre de Ruyter, wakisema kuwa serikali inakiuka wajibu wake wa kutoa umeme.

Kukatika kwa umeme kumeendelea kwa zaidi ya muongo mmoja, huku kukiwa na usimamizi mbovu na ufisadi katika kampuni ya serikali ya Eskom.

Hivi karibuni nchi imekuwa ikikosa umeme hadi saa 10 kila siku. Tatizo hilo limemfanya rais kughairi safari ya kwenda kwenye Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos ili kufanya mikutano nchini kwake na viongozi wa biashara na wafanyakazi.

Chanzo: Bbc