Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yaishtaki Israel katika mahakama ya ICJ

 Kimbari Gaza Afrika Kusini Afrika Kusini yaishtaki Israel katika mahakama ya ICJ

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afrika Kusini imefungua kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu mashambulizi ya "mauaji ya kimbari" ya utawala huo dhidi ya Gaza, ambayo hadi sasa yameua zaidi ya Wapalestina zaidi ya 21,500.

Taarifa ya kesi hiyo inasema hatua za Israel ni "mauaji ya kimbari kwa sababu zina nia ya kuleta uharibifu wa sehemu kubwa ya kundi la taifa, rangi na kaumu ya Palestina."

Aidha Afrika Kusini imesema: "Vitendo vinavyozungumziwa ni pamoja na kuwaua Wapalestina huko Gaza, na kuwasababishia madhara makubwa ya kimwili na kiakili, na kuwasababishia hali ya maisha iliyokadiriwa kuwaangamiza kimwili."

Ombi hilo limesema mashambulizi ya Israel yanakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mauaji ya Kimbari, na mahakama imetakiwa "iamuru Israel isitishe mauaji na madhara makubwa ya kiakili na kimwili kwa Wapalestina huko Gaza."

Aidha ombi la Afrika Kusini kwa ICJ limebaini kuwa "Israel imejihusisha, inajihusisha na inatishia kushiriki zaidi katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza."

Wizara ya mambo ya nje ya utawala haramu wa Israel imesema inapinga kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika mahakama ya ICJ

Chanzo: www.tanzaniaweb.live