Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yaishitaki Israel katika mahakama ya ICC

Afrika Kusini Yaishitaki Israel Katika Mahakama Ya ICC Afrika Kusini yaishitaki Israel katika mahakama ya ICC

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Afrika Kusini imeishitaki serikali ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kufuatia jukumu lake katika mzozo wa Gaza, Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumatano.

"Afrika Kusini, kama nchi nyingine nyingi duniani, tumeona inafaa kuishshtaki serikali ya Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Tumetuma rufaa kwa sababu tunaamini kuwa uhalifu wa kivita unafanywa huko," Rais Ramaphosa alisema

Hakufichua nchi nyingine zilizoshtaki Israel ICC. Aliongeza kuwa hawakuunga mkono shambulio la awali la Hamas dhidi ya Israel lakini wanapinga hatua zinazoendelea za Israel, ambazo "wanaamini kwamba uchunguzi unastahili kufanywa na ICC".

ICC ni mahakama ya kimataifa ambayo inachunguza na kuwahukumu watu binafsi wanaotuhumiwa kufanya uhalifu mkubwa unaotia wasiwasi jumuiya ya kimataifa, kama vile uhalifu wa kivita au mauaji ya halaiki.

Afrika Kusini imekuwa moja ya wafuasi wengi wa Wapalestina katika mzozo unaoendelea na Israel.

Viongozi kadhaa wa nchi hiyo wamewaunga mkono hadharani Wapalestina na pia kumekuwa na maandamano ya kuunga mkono Palestina.

Chanzo: Bbc