Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yaingia mkataba wa chanjo ya Covid

10376393 JOHNSONANDJOHNSON 660x400 Afrika Kusini yaingia mkataba wa chanjo ya Covid

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Afrika Kusini ndilo Taifa linapata changamoto kubwa barani Afrika kutokana na janga la Corona likirekodi nusu ya vifo vyote vya COVID-19 katika bara hilo na zaidi ya theluthi moja ya maambukizi yaliyoripotiwa katika bara zima la Afrika

Afrika Kusini imesaini mkataba na kampuni ya Johnson and Johnson ili kununua dozi millioni 11 za chanjo ya COVID-19 na italegeza masharti ya kupambana na janga la Corona kutokana na kupungua kwa kesi mpya, Rais Cyril Ramaphosa amesema Jana Jumapili.

Lakini maambukizi ya kila siku yalishuka chini ya elfu mbili kutoka kiwango cha elfu ishirini kwa siku kwa mwezi uliopita wakati wa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.

Rais Ramaphosa amesema katika hotuba iliyopeperushwa kwenye televisheni kwamba dozi millioni mbili na laki nane za chanjo ya Johnson and Johnson zitatolewa katika robo ya pili na zilizobaki zitasambazwa baadaye mwaka huu.

MANENO YA BASHIRU IKULU “NINGEONDOKA KESHO AU KESHOKUTWA, NIOMBEENI”

Chanzo: millardayo.com