Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yaikataa tena Israel

Israel Afrika Kusini Afrika Kusini yaikataa tena Israel

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Afrika Kusini jana Jumanne lilipiga kura ya kuunga mkono kushushwa hadhi ya ubalozi wa nchi hiyo huko Israel kutokana na kuendelea unyanyasaji na mauaji ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Sambamba na wimbi la kulaani jinai iliyofanywa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Bunge la Afrika Kusini jana Jumanne lilipiga kura ya kuunga mkono mpango wa kupunguza uhusiano na Tel Aviv.

Taarifa iliyotolewa na chama cha National Freedom Party (NFP) kilichowasilisha rasimu ya azimio hilo, imesema hatua hiyo ingeungwa mkono na kiongozi wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela.

"Huu ni wakati ambao Mandela angejivunia. Daima alisema, uhuru wetu haujakamilika bila uhuru wa Wapalestina," imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Dola la Israel liliundwa kupitia njia ya kuwafukuza wenyeji, mauaji na kulemazwa kwa Wapalestina; na ili kudumisha utawala wao, Wazayuni wameanzisha mfumo wa ubaguzi wa (apartheid) ili kuwadhibiti Wapalestina."gaza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live