Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini yaendelea kushikiria shilingi ya Israel

Israel Haina Mpango Wa Kuteka, Kukalia Au Kuitawala Gaza   Netanyahu Afrika Kusini yaendelea kushikiria shilingi ya Israel

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afrika Kusini imetoa radiamali kwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kuitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumtia mbaroni Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo kwa tuhuma za maangamizi ya kizazi.

Khumbudzo Ntshavheni, Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Teknolojia za Kidijitali wa Afrika Kusini jana alieleza kuwa: Balozi wa nchi hiyo huko Uholanzi wiki iliyopita aliwasilisha kwa mahakama ya ICC barua ya malalamiko ili kuchunguza jinai za kivita dhidi ya binadamu na maangamizi ya kizazi yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina. Jinai za Israel Ukanda wa Gaza

Ntshavheni ameeleza kuwa: Kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya jamii ya kimataifa imeshuhudia jinai zikitekelezwa dhidi ya Wapalestina ikiwemo viongozi wa Israel kutangaza waziwazi nia yao ya kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina; Afrika Kusini inataraji kuwa hati ya kukamatwa viongozi wa Israel akiwemo Netanyahu itatolewa hivi karibuni.

Waziri huyo wa zamani wa Mawasiliano na Teknolojia za Kidijitali wa Afrika Kusini ameongeza kuwa iwapo ICC haitachukua hatua mkabala wa utawala wa Kizayuni basi hilo litadhihirisha kuwa mahakama hiyo haina azma ya kuwajibika; na ni uthibitisho tosha wa kushindwa kikamilifu uongozi katika ngazi ya kimataifa na kwamba mfumo mpya wa uongozi unapasa kuasisiwa.

Msemaji wa chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC pia wiki iliyopita alisisitiza kuwa chama hicho hakipasi kujiweka kando na kutazama tu maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live