Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini wasitisha utoaji wa chanjo ya corona

Screenshot 2021 02 08 At 11.03.18 660x400.png Afrika Kusini wasitisha utoaji wa chanjo ya corona

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Afrika Kusini imesitisha kuanza utoaji chanjo ya Astra Zeneca na Oxford baada ya utafiti kuonesha chanjo hizo hazina ufanisi katika kuzuia magonjwa mepesi na ya wastani kutoka kwenye aina mpya ya virusi.

Afrika Kusini ilipokea dozi milioni moja ya AstraZeneca wiki iliyopita na ilitarajiwa kuanza zoezi la kuwachanja Wahudumu wa Afya mwezi huu. Matokeo ya awali yaashiria chanjo ya AstraZeneca inaweza isiwe na manufaa.

Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Mjini Johannesburg, yanaeleza kuwa chanjo ya AstraZeneca inatoa kinga kidogo dhidi ya aina mpya ya kirusi cha Corona.

Waziri wa Afya, Zweli Mkhize amesema chanjo ya AstraZeneca inaonekana kuwa na ufanisi dhidi ya virusi vya mwanzo lakini sio hivi vinavyojibadili na hivyo wanasitisha zoezi hilo kwa muda.

BIASHARA HATARI INAYOFANYIKA NYUMBANI KWA MTU “HII NI IKIRIPUKA HAPA NI HATARI KWA MAISHA”

Chanzo: millardayo.com