Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini na Urusi kuimarisha ushirikiano wa kijeshi – Tass

Afrika Kusini Na Urusi Kuimarisha Ushirikiano Wa Kijeshi Afrika Kusini na Urusi kuimarisha ushirikiano wa kijeshi – Tass

Tue, 16 May 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa wa ngazi ya juu wa kijeshi kutoka Afrika Kusini na Urusi wamekubaliana kuimarisha ushirikiano, na kuongeza utayari wa mapambano dhidi ya maadui zao, katika mazungumzo yaliyofanyika mjini Moscow, imenukuliwa wizara ya ulinzi ya Urusiikisema kama ilivyonukuliwa na shirika la habari linalomilikiwa na taifa hilo -Tass.

Mazungumzo ya ngazi ya juu yanakuja siku kadhaa baada ya balozi wa Marekanimjini Pretoria, Reuben Brigety, Afrika Kusini kwa kuipatia Urusi silaha na risasi, licha ya kusema kuwa haiegemee upande wowote katika vita vya Ukraine.

Kamanda wa vikosi vya ardhini wa Afrika Kusini Luteni Jenerali Lawrence Mbatha, aliongoza mazungumzo na mwenzake wa Urusi , Oleg Salyukov, mjini Moscow, limeripoti shirika la habarila Tass.

"Pande mbili zimejadili masuala ya ushirikiano wa kijeshi, na utekelezaji wa miradi ambayo inalenga kuimarisha utayari wa vita wa majeshi ya nchi mbili.

"Mkutano ujao kati ya makamanda ulifikia makubaliano kuhusu upanuzi zaidi wa ushirikiani wa vikosi vya ardhini katika maeneo mbali mbali ," ilinukuliwa wizara ya ulinzi ya Urusi ikisema.

Wiki iliyopita, Afrika Kusini ilijipata katikati ya mzozo wa kidiplomasia na Marekani baada ya Bw Brigety kusema kuwa anaamini kwamba silaha na risasi vilipakiwa katika meli ya Urusi katika ngome ya vikosi vya majini katika mji wa Capetown mwezi Disemba.

Afrika Kusini ilisema kuwa haina rekodi ya mauzo ya silaha, lakini RaisCyril Ramaphosa ameagiza uchunguzi kuchunguza madai hayo.

Katika chapisho lake la kila wiki Jumatatu, Bw Ramapphosa alisema kuwa Afrika Kusini iko chini ya"shinikizo lisilo la kawaida" la kuwa na upande inayouunga mkono katika vita vya Ukraine, lakini haitafanya hivyo katika kile ambacho ni "athari za mashindano kati ya Urusi na Magharibi".

Vikosi vya ulinzi vya Afrika Kusini (SANDF) vimethibitisha kuwa maafisa wa ngazi ya juu wako Moscow kwa sasa.

"Ni lazima ifahamike kuwa Afrika Kusini ina uhusiano wa ushirikiano nan chi mbali mbali barani na nje ya bara," SANDF kilisema katika taarifa, na kuongeza kuwa, safari hiyo ya Urusi ilipangwa vyema kabla.

Muungano mkuu wa upinzani Democratic Alliance (DA) ulisema kuwa ziara ya hivi karibuni ni mfano wa hivi karibubi wa serikali ya Afrika Kusini wa kuonyesha uungaji mkono wake kwa Urusi ‘’bila aibu’.

Chanzo: Bbc