Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kuzungumza na Uingereza, masharti ya kusafiri

Ramaphosa Pic Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Cyril Ramaphosa amesema anatarajia kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Boris Johnson baada ya Uingereza kuweka vizuizi vikali vya kusafiri kwa wasafiri wote wanaofika na kutoka Afrika Kusini.

Afrika Kusini imewekwa kwenye orodha ya nchi zilizo kwenye mstari mwekundu kufuatia kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona zilivyokithiri nchini humo, hali ambayo inawaladhimu wale wote wanao ingia Uingereza wakitokea nchini humo kukaa katika karantini maalum zilizoandaliwa kwa muda wa siku 14.

"Kitendo cha Uingereza kutuweka katika orodha hii, kimetufadhaisha kama taifa, natarajia kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Boris Johnson" Amesema Rais Ramaphosa.

Ameongeza kusema kuwa hawakutarajia kuwekwa katika orodha hiyo ambayo kwa ukubwa inaathiri sekta ya utalii inayo changia zaidi ya asilimia tatu ya pato la taifa.

"Hatuna haja ya kulipiza kisasi ... kwa sababu Uingereza ni mshirika muhimu wa kibiashara na Afrika Kusini. Rais Ramaphosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live