Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kutoa vyeti kwa waliochoma chanjo

Hati Hati Afrika Kusini kutoa vyeti vya waliochoma chanjo

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrikakusini, Cyril Ramaphosa ametangaza mpango wa kutoa cheti kwa watu waliochoma chanjo ya UVIKO-19 ikiwa ni hatua ya kukabilina na vizuizi wakati wa kusafiri.

Katika hotuba yake, Rais huyo amesema kuwa idadi ya watu watu waliopokea chanjo hiyo si kubwa kulinganisha idadi ya watu ambao bado hajwapata chanjo, na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchangamkia suala hilo ili kuweza kuokoa uchumi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuepuka madhara ya wimbi la nne la ugonjwa huo hatari.

" Baada ya wiki mbili tutatangaza utaratibu mpya wa utoaji wa hati hizi, ambazo zitatumika kama ushahidi kuonesha kuwa umepata chanjo, hii itatumika katika sehemu ambazo zinahitaji cheti cha uthibitisho"-Rais Ramaphosa.

Ameongeza kusema kuwa taifa hilo limeweza kushinda wimbi la tatu la UVIKO-19 linalosababishwa na kirusi cha Delta, na kuwa madhara katika wimbi hili hayakuwa makubwa kama ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live