Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kushirikiana na Kongo mradi wa kuzalisha umeme

Afrika Kusini Kushirikiana Na Kongo Mradi Wa Kuzalisha Umeme Afrika Kusini kushirikiana na Kongo mradi wa kuzalisha umeme

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Viongozi wanataka kufufua mradi wa kujenga mabwawa mengi kwenye mto Congo.

Viongozi wa Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametia saini karibu mikataba 40 ya kibiashara ukiwemo mmoja wa kufufua mpango wa kuzalisha umeme kwa maji.

Mradi wa Bwawa la Grand Inga ni mfululizo wa vituo saba vya kuzalisha umeme vinavyopendekezwa katika mto Kongo.

Ikiwa litajengwa kama ilivyopangwa, litakuwa ndilo bwawa kubwa zaidi la aina yake ulimwenguni.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitia saini makubaliano hayo na mwenzake Felix Tshisekedi katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa.

Afrika Kusini inakabiliwa na tatizo kubwa la umeme kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Chanzo: Bbc