Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kushauriana na Urusi hati ya ICC ya kukamatwa kwa Putin - TASS

Afrika Kusini Kushauriana Na Urusi Hati Ya ICC Ya Kukamatwa Kwa Putin   TASS Afrika Kusini kushauriana na Urusi hati ya ICC ya kukamatwa kwa Putin - TASS

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la habari la TASS limeripoti ikimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Naledi Pandor kwamba mamlaka ya nchi hii itafanya mashauriano na Urusi kuhusiana na hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin, ambayo ilitolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Hague (ICC).

Mwezi Agosti, mkutano wa BRICS (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini) utafanyika Durban, Afrika Kusini. Hapo awali, mamlaka za Afrika Kusini ziliwaalika viongozi wa mataifa yote ya jumuiya hiyo, akiwemo Putin, kwenye mkutano huo.

Wiki iliyopita, ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa Putin na mtoto wake Maria Lvova-Belova, akiwashuku kwa uhalifu wa kivita wakati wa uvamizi wa Ukraine.

Waendesha mashitaka wa mahakama wanasema huenda walihusika katika kuhamishwa kwa watoto wa Ukraine.

Tofauti na Urusi, Afrika Kusini imeidhinisha Mkataba wa Roma, ambao una maana kwamba unalazimika kuzingatia maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa Putin.

Kwa mujibu wa TASS, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alisema kuwa suala la hati hiyo litajadiliwa na Urusi.

"Tutasoma masharti ya sheria zetu, na, inaonekana, tutakuwa na majadiliano katika baraza la mawaziri , pamoja na wenzetu nchini Urusi ili kuamua jinsi ya kuendelea," Naledi Pandor alisema baada ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka ,Ali Sabri.

Siku ya Jumanne, msemaji wa Putin, Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba Kremlin "bado haijatoa uamuzi" kuhusu safari ya rais kwenda nchini Afrika Kusini.

Chanzo: Bbc