Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kupambana na vichochoro mipakani

Mkasa Wa Moto Johannesburg Ni 'janga Kubwa'   Rais Ramaphosa Afrika Kusini kupambana na vichochoro mipakani

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema, Mamlaka ya Usimamizi wa Mipaka (BMA) iliyozinduliwa hivi karibuni ni muhimu kwa ajili ya kudumisha utangamano wa mipaka ya nchi hiyo.

Kauli hiyo ya Ramaphosa imekuja huku kukiwa na ukosoaji kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu ulinzi dhaifu wa mipaka ya nchi hiyo unaoshamirisha biashara haramu ya madawa ya kulevya na uhalifu.

Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa, kuhakikisha mipaka ya nchi inasimamiwa vyema na kulindwa vyema ni muhimu kwa usalama na maendeleo.

Mpaka wa ardhi wa Afrika Kusini una urefu wa zaidi ya kilomita 4,800 na umepakana na mipaka ya nchi za Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Eswatini, na Zimbabwe.

Nchi hiyo ina bandari 53 za nchi kavu za uingiaji, viwanja vya ndege 11 vya kimataifa, na bandari nane. Mamlaka ya usimamizi wa mipaka ya BMA imeajiri mamia ya walinzi wa mpaka kulinda maeneo hayo ya kuingilia kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi.

Ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa ya Kulevya na Uhalifu 2023, iliyotolewa mwezi Juni, ilifichua kuwa Afrika Kusini imekuwa njia muhimu ya kupitisha mitandao ya wahalifu wanaojihusisha na biashara haramu ya binadamu, madawa ya kulevya, magendo ya silaha ndogo ndogo na aina nyingine za uhalifu wa kuvuka mipaka.

Ripoti hiyo ilibainisha pia kwamba Afŕika Kusini, ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa kiuchumi katika ukanda huo, inaendelea kuvutia wahamiaji wa kiuchumi ambao hawana vibali, hasa kutoka eneo la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika (SADC)..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live