Afrika Kusini, inapambana na kukatika kwa umeme, inapanga kuongeza uzalishaji mpya wa megawati 2,500 za umeme wa nyuklia.
Ni nchi pekee barani Afrika yenye mitambo ya umeme wa nyuklia wa Koeberg ulioko karibu na Cape Town, ambao unazalisha umeme nusu ya uwezo wake.
Waziri wa umeme Kgosientsho Ramokgopa amesema ongezeko la Megawatt 2,500 za nishati ya nyuklia itakuwa “ni hatua kubwa.”
Aliongeza kuwa itakuwa sehemu ya hatua zilizochukuliwa na serikali “kumaliza changamoto iliyopo ambayo nchi imekuwa ikipambana nayo” kuhusu uhaba wa umeme na wa muda mrefu wa usalama wa nishati.
Mgao wa umeme wa zaidi wa saa 12 kwa siku katika kipindi cha zaidi ya miaka 15, umeuathiri vibaya uchumi na heshima ya serikali wakati ikielekea katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.
Kampuni ya taifa ya nishati imekuwa ikikashifiwa kwa rushwa na matatizo ya matengenezo ambayo yamesababisha kukatika kwa umeme.
Katika juhudi za kuongeza uwezo wa kiwanda cha Koeberg kwa miaka 20, moja kitengo kilifungwa kwa karibu mwaka mmoja na kitengo cha pili kimefungwa wiki hii kwa jili ya matengenezo.