Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kulegeza kanuni za kudhibiti Covid-19

RAMAPHOSA Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: Jamii Forums

Rais Cyril Ramaphosa amesema Kanuni zilizowekwa kudhibiti mlipuko zitalegezwa kuanzia leo Septemba 13, 2021 kutokana na maambukizi kupungua.

Amesema japokuwa Wimbi la Tatu ambalo limechochewa na Kirusi cha Corona aina ya Delta halijaisha, Taifa hilo limeshuhudia maambukizi yakishuka katika wiki kadhaa zilizopita

Shughuli za wafanya biashara zitarudi kama kawaida ikiwemo maduka ya Pombe ambayo yalifungiwa july na wakafunguliwa kufanya biashara Jumatatu mpaka Alhamsi lakini sasa wanaruhusiwa kufanya Mpaka Ijumaa.

Ramaphosa amewataka Wananchi kujitokeza kupata chanjo akisema kuna dozi za kutosha lakini takriban watu Milioni 7 pekee kati ya Milioni 60 ndio wamechanjwa kikamilifu

Chanzo: Jamii Forums