Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini kujiondoa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC

Afrika Kusini Kujiondoa Mahakama Ya Uhalifu Wa Kivita ICC Afrika Kusini kujiondoa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Afrika Kusini anasema chama tawala cha African National Congress (ANC) kinataka nchi hiyo kuondoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Cyril Ramaphosa aliutaja uamuzi huo kuwa wa busara, ikizingatiwa kwamba - kama alivyoiweka - mahakama imezitendea baadhi ya nchi isivyo haki.

Lakini ni mchakato ambao unaweza kuchukua hadi miaka miwili.

Marekebisho yaliyopendekezwa ya sheria yatakuwa wazi kwa maoni kwa Waafrika Kusini wote kabla ya kwenda bungeni kujadiliwa.

Mahakama ya ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vyake dhidi ya Ukraine. Anasemekana kuhusika na uhamishaji haramu wa watoto wa Ukraine na kuwapeleka nchini Urusi.

Kama mwanachama wa ICC, Afrika Kusini itakuwa na wajibu wa kumkamata Bw Putin iwapo atahudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Brics Afrika Kusini mwezi Agosti.

Chanzo: Bbc