Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Watoto wala sumu ya panya wakifikiri ni pipi

Afrika Kusini: Watoto Wala Sumu Ya Panya Wakifikiri Ni Pipi Afrika Kusini: Watoto wala sumu ya panya wakifikiri ni pipi

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Zaidi ya watoto 40 walipelekwa hospitalini nchini Afrika Kusini Jumatatu baada ya kula sumu ya panya kwa bahati mbaya wakifikiri ni pipi.

"Baada ya uchunguzi wa kimatibabu, 17 walilazwa kwa uangalizi zaidi, huku 24 waliosalia wakiruhusiwa nyumbani wakiwa katika hali nzuri," mamlaka za afya za kikanda za Gauteng zilisema.

Siku ya Jumatatu pia, kundi la watu 10 wakiwemo watoto wanane walipewa rufaa kwenda katika hospitali tofauti katika mkoa huo huo.

Mamlaka za afya zinasema kuwa hii yote ni sehemu ya ongezeko "la kutisha" la jumla ya visa vya sumu ya chakula - jumla ya matukio kama hayo 863 yaliripotiwa tangu Oktoba mwaka jana.

Wanawashauri wazazi na walezi kuchukua tahadhari zaidi ili kuwalinda watoto, na wanasema mtu yeyote aliye na dalili za sumu ya chakula - kama vile kichefuchefu, kuhara, kutapika na kuumwa na tumbo - atembelee kituo cha afya kilicho karibu naye haraka iwezekanavyo.

Chanzo: Bbc