Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Waandamana kutaka kufungwa ubalozi wa Israel

Palestina Ubalozi Kusin Afrika Kusini: Waandamana kutaka kufungwa ubalozi wa Israel

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Economic Freedom Fighters, wamefanya maandamano makubwa na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina.

Waandamanaji hao waliokuwa wakipiga nara dhidi ya Israel na Marekani, walikusanyika mbele ya ubalozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria.

Kiongozi wa chama hicho, Julius Malema, kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kufungwa ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini baada ya kusisitiza kuwa, utawala wa Israel "hauheshimu ubinadamu".

Akihutubia waandamanaji hao mbele ya ubalozi wa utawala ghasibu wa Israel mjini Pretoria, Julius Malema amewataka wauzaji reja reja nchini Afrika Kusini kuondoa bidhaa zinazozalishwa na Israel kwenye mashelfu (marafu) kufikia mwisho wa Oktoba.

"Ikiwa hawataondoa bidhaa kutoka Israel, tutaziondoa wenyewe. Hatutaki bidhaa za Israel ziuzwe Afrika Kusini, hatutaki chakula kutoka kwa watu ambao wana damu ya watu wasio na hatia mikononi mwao," Alisema Bw Malema.

Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilifanya maandamano kama hayo nje ya ubalozi wa Israel siku ya Ijumaa iliyopita.

Naibu Katibu Mkuu wa ANC, Nomvula Mokonyane, alitoa wito kwa Waafrika Kusini kususia bidhaa kutoka Israel kwa mshikamano na Wapalestina.

Bi Mokonyane pia alisisitiza wito wa Afrika Kusini wa kusitisha mapigano mara moja katika Mashariki ya Kati.

Tangu kuanza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa siku 16 zilizopita sawa na Oktoba 7, kushambuliwa maeneo ya makazi na umma kwa upande mmoja na kukatwa maji, umeme na uhaba mkubwa wa chakula na dawa kwa upande mwingine, kumewafanya wakazi wa Ukanda wa Ghaza kukabiliwa na hali ngumu sana na kupelekea taasisi za haki za binadamu kutangaza hali ya kibinadamu katika eneo hilo kuwa mbaya na ya kutisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live