Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Vyama vya siasa vinavyojiandaa na Uchaguzi Mkuu

Nitasambaza Silaha Kwa Urusi   Asema Julius Malema Wa Afrika Kusini Vyama mbalimbali vya siasa vyajiandaa vema katika Uchaguzi Mkuu wa Mei 29

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mwezi mmoja kamili leo kuelekea uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini, uliopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi Mei.

Wapiga kura Milioni 27 wanatarajiwa kupiga kura, kwenye uchaguzi huo ambao chama tawala ANC kinatarajiwa kupata ushindani mkali.

Kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema, ni miongoni mwa wagombea urais na mwishoni mwa wiki iliyopita, aliendelea kufanya kampeni, Mashariki mwa jiji la Johannesburg.

"Tunaenda kupambana ili tuhakikishe kuwa tunapata ushindi tarehe 29 mwezi Mei, tutaondoa ufisadi Ikulu, huu ni wakati wenu wa kuweka historia na kuondoka kwenye shida na huu ndio wakati wetu wa kusimama imara" , amesema Julius Malema, mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha EFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live