Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Tulinufaika sana kiuchumi kwa kuandaa Mkutano wa BRICS

Brics Misri.jpeg Afrika Kusini: Tulinufaika sana kiuchumi kwa kuandaa Mkutano wa BRICS

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini kwa kifupi DIRCO imesema kuwa, manufaa iliyopata nchi hiyo kutokana na kuandaa Mkutano wa 15 wa BRICS ni makubwa kuliko gharama ilizotumia kuandaa mkutano huo.

Sehemu moja ya taarifa ya idadi hiyo imesema: "Orodha ya faida iliyopata Afrika Kusini haina kikomo. Muhimu, miongoni mwa vipaumbele vingi ambavyo Afrika Kusini ilijiwekea wakati wa mkutano huo, ilikuwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya BRICS na nchi za Afrika. Katika suala hili, viongozi wa BRICS walisisitiza uungaji mkono wao kwa Umoja wa Afrika na ajenda yake ya 2063. Aidha viongozi wa Afrika Kusini waliunga mkono ufanikishaji wa Eneo Huria la Biashara la Bara la Afrika kupitia ushirikiano wa kiuchumi na kifedha kati ya BRICS na nchi za Afrika."

Kauli hiyo ya DIRCO imekuja baada ya chama cha upinzani cha Afrika Kusini cha Democratic Alliance, kudai kuwa Afrika Kusini ilitumia randi milioni 180 (yapata dola milioni 9.7 za Kimarekani) katika kuandaa kikao hicho cha 15 cha vingozi wa kundi la BRICS.

DIRCO imejibu madai hayo kwa kusema: "Ingawa ni kweli kwamba zaidi ya randi milioni 100 zilitumika kuandaa mkutano huo lakin hazikufikia milioni 180. Vile vile faida za kiuchumi kwa Jiji la Johannesburg zinazidi kwa mbali randi milioni 100 kwa kuwa kwake mwenyeji wa mkutano huo wa BRICS."

Kwa mujibu wa taarifa hiyio, malengo mengine yaliyofikiwa kupitia mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS uliofanyika huko Afrika Kusini ni pamoja na nchi hiyo kuimarisha uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na wanachama wa BRICS ili kukabiliana na changamoto zake za umaskini, ukosefu wa ajira na ukosefu wa usawa. Changamoto hizo inaweza sasa Afrika Kusini kukabiliana nazo kupitia kuongezeka biashara ya ndani ya BRICS, uwekezaji, utalii, kuimarisha uwezo wa ndani, kutanua misingi ya teknolojia na kutumia vizuri uzoefu wa mataifa mengine ndani ya kundi la BRICS.

BRICS ni kifupi cha herufi za awali za nchi waanzilishi wa kundi hilo ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Wakati wa mkutano wa kilele wa kundi hilo uliofanyika mwezi Agosti nchini Afrika Kusini, viongozi wa BRICS walikubali uanachama wa nchi sita nyingine ambazo ni Iran, Argentina, Misri, Ethiopia, Saudi Arabia na Muungano wa Falme za Kiarabu. Uanachama kamili wa nchi hizo mpya sita utaanza tarehe 1 Januari 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live