Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Mkamateni Netanyahu na komesheni mauaji Gaza

Netanyahu Asema Wanajeshi Wa Israel Walikufa Katika 'vita Vya Haki' Afrika Kusini: Mkamateni Netanyahu na komesheni mauaji Gaza

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ameandika makala maalumu kuhusu matukio ya Ghaza na katika sehemu moja ya makala yake hiyo amesema: "Tunataraji hati za kukamatwa wahusika wakubwa zaidi wa jinai za Ghaza zitatekelezwa kama zinavyoonesha sheria za hududi kuuu za Mahakama ya Jinai ya ICC akiwemo waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Bi Grace Naledi Mandisa Pandor amesema hayo katika makala yake maalumu aliyoipa jina la "Mkamateni Netanyahu na kumesheni mauaji ya kimbari ya Ghaza."

Katika sehemu nyingine ya makala hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema: Kwa muda mrefu sana, wananchi wa Palestina wamekuwa wakinyimwa haki zao za kibinadamu na uhuru tuliopigania sana nchini Afrika Kusini. Haki hizo si za baadhi ya watu tu na wala si maalumu kwa baadhi na si haramu kwa baadhi. Bali ni haki ya kila mtu.

Sehemu nyingine ya makala hiyo ya Bi Naledi Pandor, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini inasema: Tunaeleza waziwazi kukerwa kwetu na uhalifu wa kivita unaofanywa na Israel huko Palestina, hususan kushambuliwa raia, wengi wao wakiwa ni watoto wadogo wasio na hatia, pamoja na uharibifu wa miundombinu ya kiraia, skuli za Umoja wa Mataifa, na karibu nusu ya hospitali za Ghaza. Hata katika zama za giza kuu za ubaguzi wa rangi, hatukuwahi kushambuliwa kwa mabomu katika hospitali, skuliau majengo ya makazi ya raia. Ubaguzi wa rangi Afrika Kusini ulikuwa mbaya sana kwetu kwa miongo kadhaa, lakini matukio tunayoshuhudia huko Ghaza hivi sasa ni aina mbaya zaidi ya ukandamizaji.

Vile vile amesema: Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ameanza uchunguzi wake kuhusu hali ya Palestina. Tunatoa mwito kwa Mwendesha Mashtaka huyo kuharakisha uchunguzi wa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Benjamin Netanyahu na wajumbe wa baraza lake la mawaziri. Kukosa kufanya hivyo kutachochea uvunjaji zaidi wa sheria za kimataifa na kutoheshimiwa maamuzi ya jamii ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live