Mamia ya wafuasi wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance waliandamana Jumatano kupinga kukatika kwa umeme kunakoendelea hali ambayo inazorotesha uchumi wa nchi hiyo iliyoendelea zaidi barani Afrika.
Afrika Kusini imegubikwa na tatizo la nishati kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini tatizo hili limeongekeza zaidi mwaka huu, huku nchi hiyo ikikabiliwa na ukosefu wa umeme kila siku – wakati mwingine kwa muda wa saa kumi kwa siku.
Ambao unajulika huko kama “kuelemewa kwa nishati” hivyo kukata umeme kuna maana ya kupunguza matumizi ya umeme.
Eskom, shirika la umeme la serikali lenye madeni, linakabiliwa na mitambo ya makaa ya mawe iliyochakaa ambayo inaweza kuharibika. Rushwa na hujuma pia zimelidhoofisha shirika hilo kwa kiasi kikubwa. Mkurugenzi Mtendaji, Andre de Ruyter, anatazamiwa kuacha kazi mwishoni mwa Machi.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya makao makuu ya chama tawala cha African National Congress, wakiilaumu serikali kwa kushindwa kutatua tatizo la umeme.
Mapema wiki hii, Rais Cyril Ramaphosa alisema serikali inaangalia suala la kuingiza umeme kutoka nje, lakini ameonya tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa siku moja.