Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Kampeni uchaguzi wa 2024 zaendelea

Uchaguzi Ya Afrika Kusini Afrika Kusini: Kampeni uchaguzi wa 2024 zaendelea

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC) inaendelea kusimamia kampeni za uchaguzi wa mwakani 2024 ilizozizindua jana Jumanne katika Kituo cha Mikutano cha Gallagher huko Midrand, kaskazini mwa Johannesburg, na kutangaza kuwa rasmi kuwa iko tayari kusimamia na kuenesha uchaguzi salama na wa haki.

Wakati akizindua kampeni hizo Afisa Mkuu wa Tume hiyo ya Uchaguzi ya IEC, Sy Mamabolo alisema: "Leo tunajivunia kuwa chombo mashuhuri chenye mamlaka ya kikatiba kusimamia uchaguzi na kujitolea kuwa tuko tayari kwa uchaguzi wa kitaifa na majimbo 2024. Tunakuombeni mshiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji linaloanza wiki hii na kutekeleza wajibu wenu kama wananchi wanaoshirikishwa vilivyo na wanaochagua wawakilishi wao wenyewe."

Mamabolo amesema: Kwa mara ya kwanza, watu binafsi watagombea viti katika uchaguzi wa taifa na mikoa baada ya Rais Cyril Ramaphosa kuridhia sheria mpya inayoruhusu ushiriki wa wagombea binafsi mwezi Aprili 2023. Rais Cyril Ramaphosa katika kampeni za uchaguzi

Tume ya IEC imesisitizia dhamira yake ya kufungua karibu vituo vyote vya upigaji kura na kuwataka wananchi wa Afrika Kusini kutumia tovuti na mtandao wake kujisajili, kuthibitisha ushiriki wao na kufanya masahihisho yoyote yanayotakiwa.

Aidha amesema, uchaguzi huenda ukafanyika kati ya mwezi Mei na katikati ya Agosti 2024.

Tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, uchaguzi wa mwakani 2024 utakuwa wa saba kufanyika nchini Afrika Kusini chini ya masharti ya upigaji kura kwa watu wazima na kila raia wa Afrika Kusini anaruhusiwa kushiriki kwa uhuru katika upigaji kura.

Ukiondoa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoanzia mwaka 1994 hadi 1999 na ile ya chama cha Inkatha Freedom Party iliyoanzia mwaka 1999 hadi 2004, Chama cha African National Congress (ANC) ndicho ambacho kimekuwa kikihodhi viti vingi vya Bunge tangu uchaguzi wa kwanza baada ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994, na hivyo imefanya kazi peke yake tangu wakati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live