Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini: Israel inakiuka maamuzi ya ICJ

Israel Gaza: Netanyahu Aapa Kuendeleza Mashambulizi Dhidi Ya Rafah Afrika Kusini: Israel inakiuka maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, amesema kuwa "yanayotokea katika Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na hivi karibuni huko Rafah, yanathibitisha tuhuma tulizotoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwamba mauaji ya kimbari yanatokea katika maeneo hayo ya Palestina."

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kikao cha Baraza la Utendaji la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Abab jana Alhamisi, Pandor alisema kuwa Israel inakiuka maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa kuendeleza mashambulizi yake huko Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesisitiza kwamba kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba ulimwengu umeiruhusu Israel kupuuza maazimio hayo na hakuna aliyechukua hatua yoyote, kama vile kupeleka kikosi cha kulinda amani "kuwalinda raia wasio na hatia."

Naledi Pandor pia amelaani uhalifu unaofanywa na Israel dhidi ya waandishi wa habari, akisema, "lau kama zaidi ya waandishi wa habari 170 wangeuawa katika mzozo wa Afrika, nadhani kwamba dunia nzima na vyombo vya habari vingezungumzia sana suala hilo, lakini jambo hilo linakubalika linapofanywa na Israel." Waandishi habari zaidi ya mia moja wameuawa katika mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza

Jumanne iliyopita, Afrika Kusini iliwasilisha ombi la dharura kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) la kutumia mamlaka yake kamili kusitisha operesheni ya kijeshi ambayo Israel inapanga kuianzisha katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda huko Palestina.

Hadi kufikia jana Alkhamisi, mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza yalikuwa tayari yameua shahidi Wapalestina 28,663 na kujeruhi wengine 68,395, wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Maelfu ya Wapalestina wamefukiwa chini ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa kwa makombora na ndege za kivita za Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live