Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa wa trafiki arejesha serikalini Tsh. Milioni 537 alizopata kwa rushwa

4691f292a61f92d4 Afisa wa trafiki arejesha serikalini Tsh. Milioni 537 alizopata kwa rushwa

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Afisa mmoja trafiki aliyefahamika kwa jina Jama Bare Mohamed nchini Kenya amekubali kulipa serikali KSh 26.1 milioni zaidi ya Tsh. Milioni 537 anazodaiwa kuzipata kwa njia ya ufisadi.

Jama Bare Mohamed amekuwa kortini na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) tangu mwaka 2017 Bare, afisa huyo anasemekana kupata utajiri kupitia njia isiyokuwa sawa. EACC ilisema kulikuwa na tofauti kubwa kati ya msahara wake na utajiri ulioandikwa katika jina lakeKatika njia ya kumaliza suala hilo, Bare alikubali kulipa serikali KSh 26.1 milioni

Jama Bare Mohamed amekuwa kortini na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) tangu mwaka 2017 kuhusu KSh47 milioni.

Kulingana na EACC, Bare alipata utajiri mkubwa kupitia njia isiyokuwa sawa

"Katika muda wa miaka sita, tuligundua kwamba alikuwa na mali nyingi, pesa taslimu na ardhi yenye thamani ya Sh47 milioni. Alikuwa ameweka benki Sh26 milioni, ambazo zimezuiliwa kupitia amri ya mahakama," afisa kutoka EACC alisema.

Anasemekana kuwa huwa anapokea mshahara wa kati KSh 33,050 na KSh 38,630 kila mwezi.

EACC ilishangaa namna Bare aliweza kupata utajiri mkubwa na mshahara wake mdogo ambao unaweza kuwa jumla ya KSh 2 milioni pekee baada ya miaka sita na hivyo tume hiyo mekuwa ikimwandama.

"Jumla ya Sh26,193,071 iliyokuwa katika nambari ya akaunti ya Benki ya Equity (imezuiliwa) kwa jina la Jamal Bare Mohamed be na hivyo itachukuliwa na serikali," makubaliano kati ya pande hizo yanasomeka.

EACC ilisema ilichukuwa hatua kufuatia malalamishi kutoka kwa umma kwamba Bare alikuwa akiwahangaisha na kuitisha hongo kutoka kwa madereva

Kama njia ya kusuluhisha suala hilo, Business Daily inaripoti kuwa afisa huyo alikubali kurejesha pesa hizo kwa serikali.

"Jumla ya Sh26,193,071 iliyokuwa katika nambari ya akaunti ya Benki ya Equity (imezuiliwa) kwa jina la Jamal Bare Mohamed be na hivyo itachukuliwa na serikali," makubaliano kati ya pande hizo yanasomeka.

Akijitetea, Bare alisema sehemu kubwa ya mali hiyo alirithi kutoka kwa baba yake ambaye alifariki mwaka 1987.

Bare, ambaye alianza kufanya kazi Agosti 1996, alidai kuwa alirithi ngamia 120, ngombe 80 na mbuzi 200 kutoka kwa baba yake.

Kulingana naye, wanyama hao wamezaana kuwa ngamia 217, ngombe 180 na mbuzi 268.

Mali nyingine ya utata ilikuwa kipande cha ardhi alichonunua Thika kwa KSh 3 milioni na gari.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke