Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa wa polisi aliyepotea Boni kwa siku 17 ajirejesha katika Kambi ya GSU Lamu

Eeba4fc32921b6b5 Afisa wa polisi aliyepotea Boni kwa siku 17 ajirejesha katika Kambi ya GSU Lamu

Thu, 3 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Afisa huyo aliyetambuliwa kwa jina Konstebo Norman Mwongera Kiunga alitoweka bila kupatikana kwa siku 17

- Kulingana na ripoti ya polisi Jumatano, Juni 2, afisa huyo alijiresha katika kambi ya GSU ya Basuba

- Alihamishwa kwa matibabu zaidi baada ya kurejea na majeraha ya risasi

Afisa wa polisi ambaye alitoweka kwa siku 17 katika msitu wa Boni, kaunti ya Lamu amejirejesha kwenye kambi ya GSU ya Basuba akiwa katika hali nzuri japo mnyonge.

Afisa huyo aliyetambuliwa kwa jina Konstebo Norman Mwongera Kiunga alitoweka bila kupatikana kwa siku 17 na wakati alirejea, kulikuwa na shangawe baada ya maafisa wenzake kutambua kuwa yuko hai.

Kulingana na ripoti ya Modern Corps Jumatano, Juni 2, Kiunga alikuwa na majereha ya risasi.

"Hii ni ikiwemo na risasi iliyokwama kwenye paja lake na jeraha la risasi kati ya kiwiko na kifundo cha mkono," ilisoma ripoti hiyo.

Afisa huyo bado alikuwa na silaha yake ya Negev S/No. NG7 bila risasi na pisto aina ya Ceska pistol S/no. F8526.

Kiunga alihamishwa kwa matibabu zaidi.

Tuko.co.ke iliripotia awali kuwa mwanajeshi Gershom Wanyonyi amekuwa chini ya himaya ya Al Shabaab kwa miaka mitano sasa tangu atekwe nyara 2016.

Gershom, ambaye alikuwa afisa wa KDF katika kambi ya El Adde nchini Somalia, alitekwa nyara wakati wanamgambo wa Al Shabaab waliwavamia na kumaliza zaidi ya maafisa 140.

Tangu wakati huo, familia yake haijakuwa na ripoti kumhusu hadi Al Shabaab wakatoa video akiomba usaidizi wa serikali.

Mamake, Rizpah Wasike, alisema video hiyo ni usahidi tosha kuwa mwanawe yuko hai na kuitaka serikali kufanya juhudi kumuokoa.

"Imekuwa ni miaka mitano tangu nimuone mtoto wangu. Video hiyo ni ushahidi kuwa yuko hai, naomba arejee," Wasike aliambia gazeti la Daily Nation.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke