Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa wa DCI aambia korti kondomu ilipatikana eneo la mauaji ya Sharon Otieno

Af2b2ed0d4db4e0c Afisa wa DCI aambia korti kondomu ilipatikana eneo la mauaji ya Sharon Otieno

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Vitu nane viliokotwa kutoka eneo la mauaji ikiwemo kondomu, mfuko wa kuweka kondomu, mfuko wa pombe, viatu, chupa miongoni mwa vitu vingineAfisa wa DCI aliyepiga picha eneo la tukio, Lilian Saka alisema walijaribu kuchukua alama za vidole kwenye mfuko wa kondomuAkifika mbele ya mahakama Jumanne, Julai 13, Saka alisema juhudi za kuchukua alama za vidole kwenye mfuko wa kondomu hazikufua dafu kwa sababu ulikuwa mdogo sanaHabar Nyingine: Dada Aduwaza Wageni kwa Kuhudhuria Sherehe yake ya Bathdei Ndani ya Jeneza

Katika siku ya pili ya kusikizwa kwa kesi ya mauaji ya Sharon Otieno, iliibuka kuwa polisi hawakuchukua alama za vidole kwenye vitu walivyookota mahali mwili ulipatikana.

Vitu nane viliokotwa kutoka eneo la mauaji ikiwemo kondomu, mfuko wa kuweka kondomu, mfuko wa pombe, viatu, chupa miongoni mwa vitu vingine.

Afisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) aliyepiga picha eneo la tukio, Lilian Saka alisema walijaribu kuchukua alama za vidole kwenye mfuko wa kondomu.



Read also

Bibi Mwenye Umri wa Miaka 90 Aliyepigana na Saratani Ambaye Hukimbia Kilomita 10

Hata hivyo, akifika mbele ya mahakama Jumanne, Julai 13, Saka alisema juhudi za kuchukua alama za vidole kwenye mfuko wa kondomu hazikufua dafu kwa sababu ulikuwa mdogo sana.

Katika kuipa uzito ushahidi wao baada ya kushindwa kuchukua alama za vidole, upande wa mashtaka uliwasilisha picha 213 zilizokuwa zinaonyesha eneo la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo.

Katika kesi hiyo, Gavana wa Migori Okoth Obado, msaidizi wake Michael Oyamo na Casper Obiero wanatuhumiwa kumuua Otieno na mwanawe aliyetarajia kumzaa.

Kisa hicho kilitokea mnamo Septemba 3, 2018, ndani ya Msitu wa Kodera katika kaunti ya Homa Bay.

Kuahirishwa kwa kesiWiki kadhaa iliyopita, Obado kupitia wakili wake Kioko Kilukumi, alimwandikia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji barua akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo.

Obado alitaja mlipuko wa COVID-19 kama kizingiti kwake kusafiri Nairobi.

Hata hivyo, ombi la Obado lilikataliwa na upande wa mashtaka.



Read also

Dada Aduwaza Wageni kwa Kuhudhuria Sherehe yake ya Bathdei Ndani ya Jeneza

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke