Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa afutwa kazi kwa kumpa uraia Mchungaji Bushiri aliyekimbia Malawi

Shepherd Bushiri And Daughter?fit=700%2C448&ssl=1 Mchungaji Bushiri

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa wa Afrika Kusini aliyeidhinisha ukazi wa kudumu kwa mchungaji wa Malawi mwenye utata Shepherd Bushiri amefukuzwa kazi. Kufutwa kwake kulifuatia mchakato wa kinidhamu uliochukua takriban mwaka mmoja.

Ronney Marhule alipatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kutofuata sheria za uhamiaji kwa kutoa vibali kwa familia ya Bw Bushiri ambavyo "havikustahili", idara ya masuala ya ndani ilisema.

"Matokeo ya kikao hiki cha kinidhamu yanatupeleka karibu na kuhakikisha kwamba tunakomesha vitendo na maamuzi yasiyo ya kawaida ya maafisa wa masuala ya ndani ndani ya mfumo," Waziri wa Mambo ya Ndani Aaron Motsoaledi amenukuliwa akisema na vyombo vya habari vya ndani.

Bushiri, anayejiita "nabii", na mkewe Mary wanakabiliwa na mashtaka ya ulaghai nchini Afrika Kusini, lakini walikimbilia Malawi baada ya kupewa dhamana.

Hati ya kukamatwa ilitolewa na taratibu za kuwarejesha nchini Malawi zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live