Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki wakati akiruka ghorofani huku akirekodiwa

Ghorofaaaa (29).jpeg Afariki wakati akiruka ghorofani huku akirekodiwa

Tue, 16 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 23 ambaye alirekodiwa akiruka kutoka kwa jengo la ghorofa nne katika mji wa Mombasa alifariki katika Hospitali Kuu ya Pwani baada ya kukimbizwa huko kwa matibabu siku ya Jumatatu asubuhi.

Katika video ya tukio hilo ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwathiriwa anaonekana akiruka kutoka kwenye dirisha lililo wazi la hoteli moja katika eneo la Bondeni, kando ya barabara ya Abdel Nasser.

Alikuwa amejifunga taulo jeupe kiunoni wakati alijiachia na kuanguka chini kwa kishindo.

Wakati akithibitisha kifo cha mwanamume huyo anayeshukiwa kujirusha katika jaribio la kujitoa uhai, Kamanda wa Polisi wa kaunti ya Mombasa Stephen Matu alithibitisha kuwa marehemu alifariki katika hospitali kuu ya Pwani kutokana na majeraha ya ndani kichwani na tumboni.

Kulingana na ripoti ya polisi, mwanamume huyo ambaye ni raia wa Somalia aliruka kutoka kwenye dirisha la hoteli lililokuwa wazi na kutua kwenye barabara kwa kishindo ambapo alilala bila fahamu kabla ya wasimamizi wa hoteli hiyo kumkimbiza hospitalini. Iliripotiwa kuwa alikufa baadaye mwendo wa saa nne unusu asubuhi.

Polisi baadaye walifanya upekuzi kwenye chumba cha hoteli cha mwanaume huyo na kugundua kwamba alikuwa ameharibu vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na TV, mapazia na taa.

Kulingana na ripti, familia ya marehemu ambayo inaishi Nyali ilikuwa imempangia chumba katika hoteli hiyo baada ya kuanza vurugu. Uchunguzi wa kifo cha mwanaume huyo bado unaendelea na polisi wanatafuta kubaini sababu ya tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live