Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki akipigana na kaka yake kuhusu kupika

Crime Scene Decoration  Mw 133583 2 Afariki akipigana na kaka yake kuhusu kupika

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msiba umegubika familia moja katika kijiji cha Ikorongo, kata ya Miruka, Kaunti ya Nyamira, baada ya mvulana wa miaka 15 kumuua kakake kwa kuzozania jukumu la kupika.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira Kusini (SCPC) Moses Kirong’ alithibitisha mkasa huo. Picha: UGC. Chanzo: UGC

Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira Kusini (SCPC) Moses Kirong’ baada ya naibu chifu wa kata ya Miruka Robert Maugo kupiga ripoti kuhusu tukio hilo.

Ripoti zinasema kwamba kaka hao wawili walikuwa na mdogo wao wakipika wali walioachiwa na bibi yao wale mchana wakati hakuwa.

Kwa mujibu wa Kenya News Agency, kila mmoja alikuwa na zamu ya kuangalia iwapo wali umeiva, ila kaka yao mdogo alikataa jukumu hilo na vita vikaibuka na kusababisha kifo.

“Wakati zamu ya mwendazake ilipowadia ya kuangalia wali uliokuwa jikoni, alikataa hadi kakae mkubwa akasisitiza ila hakukubali na kundelea kucheza na kaka yake mdogo wa miaka 7,” naibu chifu alisimulia.

Kirong’ alisema kulinaga na kakake mdogo aliyeshuhudia tukio hilo, mwendazake alipigwa kwenye kifua wakati wa fujo hizo na kupotza fahamu baada ya kugongwa ngumi kwenye mbavu.

Mkuu huyo wa polisi alisema hatimaye kaka hao wawili waligundua kwamba amezirai na, kaka mkubwa akajaribu kumfufua ila haikufua dafu, hata alipomwagia maji baridi mwilini mwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live