Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AfDB yazindua dhamana ya kijamii ya Kangaroo ya dola milioni 464

3f4f9178eb47384d2d3348af61ca3884.jpeg AfDB yazindua dhamana ya kijamii ya Kangaroo ya dola milioni 464

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema inarejea kwenye soko kuu la hisa la Australia kwa kuzindua dhamana ya miaka 5.5 ya Kangaroo ya kijamii yenye thamani ya dola milioni 464 (Shilingi trilioni 1.076).

Hii inakua mara ya pili kwa benki hiyo ya maendeleo kuzindua dhamana ya aina hii, ambapo mwaka jana ilizindua dhamana ya miaka mitatu yenye thamani ya dola biliono 3.1 kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

AfDB imesema katika taarifa yake kuwa kiwango hicho cha pesa kitatumika kusaidia kuboresha upatikanaji wa umeme, maji na usafi wa mazingira, na mipango mingine ya kijamii barani Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz