Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AfDB yatoa fedha ujenzi wa  barabara ya Kampala-Jinja

AfDB1 AfDB yatoa fedha ujenzi wa  barabara ya Kampala-Jinja

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI ya Maendeleo Afrika (ADB) na serikali ya Uganda wamesaini mkataba wa makubaliano ya ufadhili wa dola za Marekani milioni 229.5 kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara ya Kampala-Jinja.

Barabara hiyo pia itapunguza muda wa kusafiri na kukuza biashara kwenye maeneo muhimu inayounganisha Uganda na nchi za jirani.

Awamu ya kwanza ya mradi huo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ya Kampala-Jinja (PPP) utaboresha usafiri na kupunguza muda wa kusafiri kutoka zaidi ya saa tatu hadi chini ya saa moja kati ya miji hiyo.

Waziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi, Matia Kasaija alisaini makubaliano hayo kwa niaba ya serikali na kueleza kuwa kuwa Benki ya Maendeleo Afrika ni wafadhili wa pili kimataifa wanaochangia asilimia 20 ya misaada ya maendeleo katika maeneo ya barabara, nishati, kilimo, elimu, afya na usafi wa mazingira.

Alisema barabara ya Kampala-Jinja ni lango kuu la bidhaa zinazoingia na kutoka nchini na utekelezaji wake ukifanikiwa utachochea biashara na ukuaji wa uchumi na nchi za jirani.

Meneja wa Benki hiyo nchini Uganda, Augustine Kpehe Ngafuan alisema makubaliano hayo yanaonyesha kujitolea kwa benki hiyo kusaidia maendeleo ya nchi na kuimarisha ustawi wa watu wake.

Ufadhili wa mradi huo ni sehemu ya kujitolea ya benki hiyo kuboresha hali ya maisha ya watu wa Afrika kupitia ujumuishaji wa kikanda na inaambatana na mkakati wake wa miaka 10 (2013-2022) kwa Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz