Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake chooni akimdai fedha

MAITI YAPOTEA Adaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake chooni akimdai fedha

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Ismail Chelangat (20), ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya kilimo katika Chuo cha Uganda Christian kilichopo mji wa Lira nchini Uganda anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumuua mwanafunzi mwenzake.

Tovuti ya Daily Monitor imeripoti kuwa Aprili 14, mtuhumiwa alimchoma kisu Jeremiah Mwanga (24) hadi kufa, akimtuhumu kushindwa kurejesha pesa alizomkopesha.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi wa eneo hilo, Patrick Okema amesema kwa sasa mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kapchorwa.

Okema amesema baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbilia katika Wilaya ya Kapchorwa ambapo ndipo alipokamatiwa.

Chanzo: mwanachidigital