Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kujiua kwa kujifyatulia risasi akisubiri matibabu

Kifo Kifo Mauiaji.png Adaiwa kujiua kwa kujifyatulia risasi akisubiri matibabu

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee mwenye umri wa miaka 72, Amos Mohamed amedaiwa kujipiga risasi na kujiua alipokuwa akisubiri matibabu katika hospitali moja eneo la Kusini B, Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Star ya nchini humo, mzee huyo alimtembelea wakili wake kabla ya kuagiza teksi ya kumpeleka hospitali.

Polisi wa eneo hilo wameanzisha uchunguzi baada ya mzee huyo kujifyatulia risasi na kujiua papo hapo katika mazingira ya kutatanisha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha Mohamed alijipiga risasi akiwa kwenye kiti cha nyuma cha gari lililompeleka hospitali.

Mwanamume huyo inadaiwa alikuwa akisubiri matibabu ya ugonjwa ambao haujajulikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live