Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Acheni kuiletea Afrika aibu na kejeli’-Mseto wa maoni mapigano Sudan

Mawaziri Wa Mambo Ya Nje Wa Marekani Na Uingereza   Antony Blinken Na James Cleverly 'Acheni kuiletea Afrika aibu na kejeli’-Mseto wa maoni mapigano Sudan

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Kumekuwa na msururu wa maoni na wito wa kusistishwa kwa mapigano nchini Sudan kutoka nchi mbali mbali za Afrika na duniani kote .

Tazama walichosema viongozi wa Afrika na mataifa mengine.

·Afrika Kusini : Ilitaja hali ya Sudan kuwa "ya kusumbua" na kutoa wito kwa pande zinazopigana kuwaepushia watu wa Sudan machafuko yoyote zaidi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

·Uganda : Rais Yoweri Museveni alisema ni "muhimu zaidi" kusitisha uhasama "kukomesha maafa na kejeli kwa Afrika"

·Kenya : Rais William Ruto aliwataka viongozi wa kanda kuchukua msimamo thabiti kurejesha amani Khartoum. Mamlaka ya Kenya inasema inapanga kuwahamisha raia wake 3,000 waliokwama nchini Sudan

·Ethiopia : Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema mapigano hayo "yanakinzana na kanuni na maadili ya Sudan ya muda mrefu na yenye mizizi mirefu"

·Chad : Baraza tawala la kijeshi limefunga mpaka na Sudan na kuwataka "wanaopigana waanze mazungumzo"

·Guinea-Bissau : Rais Umaro Sissoco Embalo - ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas) - vile vile ametoa wito kwa utulivu na mazungumzo.

·WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema watu nchini Sudan wanataka "wanajeshi warudi kambini" na kutoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa ghasia hizo.

·Uingereza : Waziri wa Mambo ya Nje James Cleverly alisema mustakabali wa Sudan "hatimaye uko mikononi mwa majenerali wanaohusika katika vita hivi", na kuwataka kuweka amani mbele.

·China : Imesema inafuatilia kwa karibu hali hiyo na inatumai "vyama nchini Sudan vitaongeza mazungumzo na kuendeleza kwa pamoja mchakato wa mpito wa kisiasa"

·Urusi : Ilionyesha wasiwasi wake juu ya "matukio makubwa yanayotokea Sudan," na ilitoa wito kwa pande zinazozozana kuonyesha nia ya kisiasa na kujizuia.

·Ujerumani : Ilisema kamati ya mgogoro ilikuwa imeitishwa na ilikuwa ikifuatilia matukio kwa karibu

·Umoja wa Mataifa: Umelaani kushindwa kwa pande zote mbili kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu

Chanzo: Bbc