Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ijumaa alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mahasimu wawili wakuu katika vita vya sasa ambao ni Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.
Mazungumzo hayo ya simu yalilenga kujadili njia za kusuluhisha tofauti kwa njia ya kirafiki na kuleta utulivu nchini Sudan.
Waziri Mkuu Abiy aliandika katika ukurasa wake wa Twitter baada ya majadiliano yake na pande zote mbili kwamba: "Nimefanya mazungumzo ya simu na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo juu ya haja ya kusuluhisha tofauti kwa amani na kuleta utulivu nchini Sudan,"
Abiy aliongeza kuwa, "watu wakuu wa Sudan wanastahili amani,"
Jenerali Dagalo, kiongozi wa Kikosi cha Wanajeshi wa Msaada wa Dharura (RSF), aidha aliandika katika Twitter kwamba amefanya mazungumzo yake ya simu na kiongozi huyo wa Ethiopia.
"Nilifanya mazungumzo yenye tija na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed Ali, ambapo tulizungumzia masuala mbalimbali ya mgogoro unaoendelea nchini Sudan na kubadilishana mawazo kuhusu mgogoro wa sasa."
Kwa mujibu wa Dagalo, waziri mkuu wa Ethiopia alisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhu la mgogoro wa Sudan.
Mazungumzo hayo ya simu yalikuja wakati Ethiopia inaripotiwa kujaribu kupatanisha pande zinazozozana kwa ushirikiano wa kikanda na IGAD na Umoja wa Afrika.
Wiki mbili zilizopita, Sudan iliingia katika mgogoro mkubwa kutokana na kuwania madaraka majenerali hapo wawili wenye nguvu zaidi wanaoongoza vikosi tofauti vya kijeshi.
Tangu kuzuka kwa mzozo wa Sudan, zaidi ya watu 500 wameuawa na zaidi ya 4,000 katika mapigano hayo baina mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan ambaye pia ni mtawala wa nchi hiyo na naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo, kamanda wa kikosi chenye nguvu cha msaada wa dharura (RSF) ambaye ni maarufu kwa jina la Hemeti. RSF ni kikosi chenye nguvu kilichoundwa na wanamgambo wa Janjaweed ambao kwa miaka mingi walihusika katika mapigano ya mkoa wa magharibi wa Darfur.